Maana ya kuokoka,(wokovu ni nini)

BALOZI ANANINI LA KUSEMA JUU YA NENO MAANA YA KUOKOKA? 
MAANA YA WOKOVU:   wengi neno hili wamelitafsiri vile wa pendavyo au waonavyo  sasa Swali hili acha lijibiwe na maandiko matakatifu, na maneno haya yasibadilishwe kwamba ni wakati gani wa kuokoka kitendo kikishamalizika cha kukiri kifuatacho ni uwokovu kwa mjibu wa neno, fuatilia hapa chini,
Kwasababu ukimkiri Yesu  Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe yote! “Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”. Wengine hudhani kuokoka ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani ya kujinyima raha na kujitenga na jamii.
Wengi hudhani wokovu ni maisha duni na ya umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna tafsiri nyingi  sana tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi ni mitazamo tu  ya mwanadamu kumtafuta Mungu na hajampata. Unaweza ukaangalia tafsiri nyingine iliyorahisishwa kabisa, kukupa wewe msomaji kuelewa maana halisi ya maana ya Kuokoka
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani. Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,
Mfano:- kwa kila neno nililoliorodhasha hapo,
- Kunusurika; Paulo aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita, alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika,
 basi tukakata tamaa ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu, hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo, akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea, wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama. Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
 Hivyo tunaona “KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke msalabani. ( Mk 15:30)
Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kasha ukadhibitishwa kwetu na wale waliosikia. (Ebr 2:3)
KUOKOKA” katika mistari hii imetumika kama “KUPONA”.
“Na niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni, na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za Manabii; Ambao kwa imani, walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
- KUOKOKA katika mistari hii, imetumika kama KUPONA, KUSALIMIKA AU KUNUSURIKA!
- Kusalimika; Wakati Mungu anaangamiza dunia kwa maji ya gharika, Biblia inasema;
“Wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu mjumbe wa haki na watu
wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasio mcha Mungu. Tena
akaihikumu miji ya sodoma na Ghomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya
akaifanya iwe ishara, kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya hayo.
Akamwokoa Lutu, yule mwenye haki, aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi  wa hao wahalifu. (2Pet 2:5-7)
“Hapa KUOKOKA” imetumika kama “KUSALIMIKA” kutoka katika janga la gharika na moto.
- Kufunguliwa au Kukombolewa;
 Herode alipomtia Petro gerezani ili amuuwe, Biblia inasema;
Panapo majira yale yale, herode mfalme akanyoosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamuuwa Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga. Na akiona yakuwa imewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamshika na Petro … akamweka gerezani, akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde,
Akitaka baada ya Pasaka, kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa lilikuwa likimwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule, Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, alikuwa amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi! Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo.
Kisha akamwambia, jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua yakuwa ni kweli, yaliyofanywa na malaika. Bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema,
“sasa nimejua yakini yakuwa, Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi”. Na alipokuwa akifikiri hayo, akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana Marko … na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Naye alipobisha, kijakazi jina laki Rhoda akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya Petro, hakufungua mlango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani, akawaambia kwamba, Petro anasimama mbele ya lango. (Mdo 12:1-14-19)
“KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUFUNGULIWA” au “KUKOMBOLEWA” katika kifungo.

UHAKIKA WA WA NENO WOKOVU
Kwahiyo KUOKOKA ni KUNUSURIKA, KUSALIMIKA, KUKOMBOLEWA, KUFUNGULIWA au KUPONA kutoka katika JANGA au HATARI fulani.
Yesu alikuja kuleta wokovu (kuokoa) na Biblia inataja mistari mingi sana juu ya koukoka au wokovu.
Kwa mfano:-
  • Yoh 3:16-18;   Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyehamini amekwisha kuhukumiwa;
  • kwa sababu hakuliamini jina la mwanawe wa pekee.
  • Luk 9:59;   Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa,
  • Yoh 12:47; Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi si mhukumu, maana sikuja niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
  • 1Tim 1:15; Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa ya kwamba, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
  • 1Tim 2:14; Mungu … hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yalio kweli.
  • Efe 2:5,8; Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo, yaani, mmeokolewa kwa Neema, Kwa maana mmeokolewa  kwa Neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
  • 1Kor 1:18; Kwa sababu neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
  • Mdo 4:10-12; Jueni nyote na watu wote wa Israel ya kuwa, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu … kwa jina hilo mtu huyu anasimama Hali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
  • Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47; Enyi waume wa Israel, sikilizeni maneno haya: Yesu wanazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; ambaye Mungu alimfufua, akifunga uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao…
Basi nyumba yote ya Israel nawajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akamwambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu,
nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa watu wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi …
Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
(Mdo 2:22-24,    36-40,    43-44, 47)
Rum 10:9-10; Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, nakuamini mioyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Mdo 16:30-31; Kisha akawaleta nje akasema. Bwana zangu, Yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
2Kor 6:2; Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusukia, siku ya wokovu nalikusaidia; Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; Tazama, siku ya wokovu ndio sasa.
Ebr 2:1-3; Kwa hiyo, imetupasa kuangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa, kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika, lilikuwa imara, na kila kosa na uasi, ulipata ujira wa haki. Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitika kwetu na wale wanaosikia.
AWALI TULIKUWA WAPI NA TUNAFANYA NINI
1.    Tumeokolewa kutoka katika Nguvu ya Dhambi yaani uasi,
Maana sijui nifanyalo; kwasababu lile nilipendalo silitemdi; Bali lile nilichukialo ndilo nilitendalo … naikiri kuwa ile sheria ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo,
 Bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua kuwa, ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema, kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati … lakini katika viungo vyangu, naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, masikini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukru Mungu  kwa Yesu kristo  Bwana wetu R7:15-
Nanyi mlikuwa wafu kwasababu ya makosa na dhambi zenu. Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuaata Mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tama za miili yetu, tulipo yatimiza matendo ya mwili na nia, kukawa kwa tabia yetu watoto wahasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema akatufufua pamoja naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”(Efe 2:1-1-2-6)
Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”. (Rum 8:1-2) … “tukijua neno hili, ya kuwa, utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike. Tusitumikie dhambi tena …
Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu … kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mli-itii kwa mioyo yenu, ile namna ya elimu (Injili ya wokovu), ambayo mliwekwa chini yake. Na mlipokwisha kuwa huru mbali na dhambi,
Mkawa watumwa wa haki … kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayo yatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima. … Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa. (Ezek 28:20-23) … kwa maana mshahara wa dhambi nimauti wa milele, bali karama (zawadi) ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum 6:23)
Pia soma; Tito 2:11-12; Tito3:3-4; 2Kor 4:3-4; Efe 4:18-19; 1Tim 1:13-15
2.  TUMEOLOKEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake”. (Kol 1:13)
“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, mliwafanya hai pamoja naye, akisha kutusamehe makosa yote;
akisha kuifuata ile hati iliyoandikwa kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi za mamlaka, na kuzifanya kwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo”. (Kol 2:13-15)
Tazama, nimwewapa amri ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. (Luk 10:19)
 Math 27:45,50-54; Ebr 2:14-15; Luk 11:21-22; Yoh 19:28-30
Je? umewahi kujiuliza swali hili kwanini Tunaishi?  swali hili limekuwa na majibu mengi sana, kutokana na vile wanavyo fahamu au wanavyojuwa  majibu hayo yanaweza kuwa sawa, na yanaweza kuwa ya kweli,
lakini inapendeza sana tunapowaza kuhusu Mungu tukawaza pole pole, ili kupata kile kilichokusudiwa